Baada ya kuchumbiwa kwa muda mrefu na kushindwa kukamilisha hatua iliyopaki ya ndoa, baadhi ya mashabiki wa mwanamuziki Avril, wamekuwa na maswali mengi huku wakitaka kujua kama ndoa ipo au la.
Kwa mujibu wa mwanamuziki huyo wa Kenya, amedai kuwa taratibu za kuchunguza uhalali wa familia ya mchumba wake ambaye ni raia wa Afrika Kusini, ndiyo uliochelewesha ndoa hiyo baada ya kuvishwa pete ya uchumba Novemba mwaka jana.
Amedai kuwa taratibu zaidi za ndoa huhusisha wazazi, na kudai kuwa pande mbili zikikubaliana hatua hiyo huenda vizuri na sio kukurupuka wao wawili bila kuwahusisha wazazi.
Mwanadada huyo amedai kuwa Mungu, akijalia ndoa itakuwa mwezi ujao ‘Disemba’ mwaka huu, ambapo kwa sasa mwadada Avril, ameachia kazi mpya ‘No Stress’ akiwa amemshirikiasha rapa AY na muongozaji Hanscana kutoka Tanzania.

Post a Comment