Ndoto za watanzania kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi, zilisitishwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Mustapher Tchaker mjini Blida, Algeria, kufuatia Stars kukubali kipigo cha bao 7-0 toka kwa timu ya taifa ya Algeria.
Stars imetupwa nje ya mashindano kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya mchezo wa awali timu hizo kutoka sare ya kufungana kwa magoli 2-2 kwenye mchezo uliochezwa November 14 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Algeria, dhidi ya Taifa Stars (Tanzania) kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa, inadaiwa kuwa hayuko katika hali nzuri ya kuzungumza chochote na kuomba kuzungumza kwenye uwanja wa ndege wa Algiers kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Ni kawaida kwa makocha na manahodha wa timu kuzungumza mara baada ya mchezo kumalizika na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari ambayo huulizwa kuhusiana na mchezo husika.

Post a Comment