Ikiwa bado siku kama 60 kuweza kufikia January ya mwaka 2016 wakati ambao vilabu kadhaa barani Ulaya
vitakuwa vikihusishwa kusajili wachezaji kutokana na kuwa ni wakati
ambao dirisha dogo la usajili litakuwa limefunguliwa, klabu ya Liverpool ya Uingereza tayari imeanza kunyemelea huduma ya mshambuliaji wa kibrazil Alexandre Pato.
Alexandre Pato ambaye amewahi kuchezea klabu ya AC Milan ya Italia kwa sasa anacheza klabu ya Sao Paulo kwa mkopo akitokea klabu ya Corinthians na anatajwa kurudi Corinthians mwezi January 2016 ila klabu hiyo inataka kumuuza kutokana na kutaka kupunguza mzigo wa gharama kwa klabu.
Kupitia kwa Rais wa klabu ya Corinthians Roberto De Andrade
amethibitisha kutaka kurejea kwa mshambuliaji huyo mwezi January ila
wamemuweka sokoni, licha ya kuwa amesema hakuna klabu ambayo imeomba
kujua bei ya mshambuliaji huyo ambaye anatajwa kufikia thamani ya euro
milioni 25 na amefunga jumla ya magoli 26 kwa mwaka 2015 katika
mashindano yote aliyocheza.
“Ndio
tunataka kumuuza Pato, tunajua ni ugumu kiasi gani utakuwa kwa upande
wetu wakati atakaporejea na sina uhakika kama tutafanikiwa kumuuza
ila Corinthinans bado haijapokea ombi kutoka katika klabu yoyote ya
kutaka kujua bei ya mchezaji huyo ila wakala wake anafanya mazungumzo na
vilabu vya Ulaya kwa ajili ya uhamisho”>>> Roberto De Andrade
Hata hivyo uchunguzi uliyofanywa na vyombo vingi vya habari za michezo ni kuwa klabu ya Liverpool ndio inahusishwa kwa karibu kutaka kumsajili Alexandre Pato hususani kauli ya Rais wa Corinthians Roberto De Andrade kutaja kuwa wakala wa mshambuliaji huyo anafanya mazungumzo na vilabu vya Ulaya.

Post a Comment